Print
Hits: 2532

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRIME MINISTER’S OFFICE
(POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENT)


 “THE REVIEW OF THE NATIONAL INVESTMENT PROMOTION POLICY OF 1996”

NATION-WIDE CALL FOR INPUTS


The Government of the United Republic of Tanzania through the Prime Minister’s Office (Policy, Coordination and Investment) is undertaking the review of the National Investment Promotion Policy (NIPP) of 1996. This policy was formulated as part of the Government efforts in addressing the challenges facing the country in meeting its socio-economic aspirations given the resources and other intangible advantages that it enjoys. In addition, the review has been necessitated by various business and investment changes in the global, regional and national spheres since its inception in 1996. Moreover, the review will among others, form the basis for the formulation of the new National Investment Policy and its Implementation Strategy so as to align with and accelerate the realization of the aspiration of attaining the mid-income country as per Tanzania Development Vision 2025. Either, the process will sustain the country in optimizing the opportunities arising from the attainment of the middle income economy status.

Additionally, the Policy review process is embracing the principles of transparency, inclusiveness and consultation with all nationwide stakeholders. In that regard, the Government is hereby inviting the general public to submit their views, opinions and recommendations to foster the review process. The inputs provided will be treated with complete confidentiality and confined to this process only.
Inputs are invited, but not limited to the core areas identified here under:

1.    Effective utilisation of national endowment
2.    Mobilization of domestic and international financing for investments
3.    Provision of enabling physical infrastructure (Water, Electricity, Energy, Roadway, etc)
4.    Improvement of export competitiveness
5.    Institutional framework to support investment development
6.    Land acquisition and ownership for investment
7.    Regulatory Framework including licensing, permits and approval processes for investment
8.    Human capital development
9.    Technological advancement and adoption
10.    Investment incentives
11.    Legal and Institutional Framework for investment
12.    Bilateral and Multilateral Investment Agreements and Treaties  
13.    Investment Disputes Settlements  

Kindly submit your inputs to Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. or Postal Address: Permanent Secretary, Prime Minister’s Office, (Policy, Coordination and Investment), P.O BOX 980, Government City, Mtumba, DODOMA not later than 20th September, 2019.

THANK YOU FOR DEVOTING YOUR VALUABLE TIME FOR THIS IMPORTANT NATIONAL ENDEAVOUR

 

__________________________________________________________________________________________

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
    OFISI YA WAZIRI MKUU    
(SERA, URATIBU NA UWEKEZAJI)

 “MAPITIO YA SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 1996”
WITO WA KUPATA MAONI KUTOKA KWA UMMA  

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) inafanya Mapitio ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996. Sera hii ilitungwa ikiwa ni sehemu mojawapo ya  jitihada za Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi katika kufikia matumizi bora ya rasilimali zake ili kuwezesha kunufaika na kufikia malengo yake ya kiuchumi na ya kijamii. Mapitio haya yanafanyika kutokana na mabadiliko mbalimbali ya mazingira ya biashara na uwekezaji katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa tangu kutungwa kwake. Aidha, mapitio haya pia yatawezesha kutungwa kwa sera mpya ya uwekezaji na kuandaa mkakati wa utekelezaji utakaowezesha nchi kufikia malengo ya nchi ya kipato cha kati kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa haraka na kutumia ipasavyo fursa zilizopo na zinazojitokeza. Vile vile, kazi hii inazingatia dhana ya uwazi na ushirikishwaji wa wadau wote muhimu.


Hivyo, Serikali inatoa wito kwa umma kuwasilisha maoni na mapendekezo yao ili kufanikisha zoezi hii. Maoni yatakayotolewa yatakua siri na yatatumika kwa ajili ya kufanikisha malengo ya zoezi hili pekee. Maoni yatumwe kabla ya tarehe 20 Septemba 2019 kupitia barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au njia ya Posta kwa: Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) S.L.P 980, Mji wa Serikali, Mtumba, DODOMA. Maoni yanaweza kuhusisha maeneo yafuatayo:


1.    Matumizi bora ya rasilimili za nchi
2.    Upatikanaji wa rasilimali fedha na mitaji kutoka ndani na nje ya nchi
3.    Upatikanaji wa miundombinu wezeshi ya uwekezaji (Maji, Umeme, Nishati, Barabara, n.k)
4.    Kuimarisha ushindani wa mauzo ya nje ya nchi
5.    Mifumo ya kitaasisi ya kuwezesha na kukuza uwekezaji
6.    Upatikanaji na umiliki wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji
7.    Mifumo ya udhibiti wa biashara na uwekezaji
8.    Maendeleo ya Rasilimali Watu
9.    Maendeleo ya Teknolojia na matumizi yake
10.    Vivutio vya Uwekezaji
11.    Mifumo ya kisheria ya kuvutia, kuwezesha na kukuza uwekezaji
12.    Mikataba ya kimataifa ya uwekezaji
13.    Mifumo ya usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji


“AHSANTE KWA KUTENGA MUDA WAKO ADHIMU KUFANIKISHA ZOEZI HILI MUHIMU LA KITAIFA”

4 Septemba 2019