WAZIRI MKUU AKUTANA NA UONGOZI WA BODI YA MISHAHARA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, ameitaka ifanye kazi kwa bidii.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, ametolea mfano kada ya elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

Amekutana na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Dolnad Ndagula leo (Alhamisi, Januari 24, 2019) pamoja na baadhi ya wajumbe kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bidi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kubotesha utendani wa watumishi wa umma nchini.

Serikali inaimani kubwa kwa wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye  utumishi wa umma.

“Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”

Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi.

-ends-