Logo
MHAGAMA: Amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukamilisha Ujenzi wa Barabara ya KM 15.
Thursday, 15 December 2016 08:06    PDF 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Hemed Mwanga kuhakikisha anatatua mgogoro wa ujenzi wa Barabara ya Kiwangwa- Mambohela yenye urefu wa kilometa 15 ndani ya mwezi huu.

Ameyasema hayo tarehe 15 Desemba, 2016 wakati wa ziara kikazi Wilayani Bagamoyo alipotembelea Ujenzi wa Soko la Magomeni na Barabara ya Kiwanga - Mabohela ikiwa ni miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Bagamoyo kwa ufadhili wa Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

“Utaratibu wa Mradi wa MIVARF haina fidia, tumeshajenga barabara katika Halmashauri 76 nchi nzima bila ya kuwa na fidia hivyo anashangaa kuona ni kwanini wananchi barabara ya Kiwangwa – Mabohela wanadai fidia kwa kipande cha KM 1.6 imeachwa bila kukamilishwa”.

“Nakugiza Mkuu wa Wilaya ukae na Timu yako ya Bagamoyo na Chalinze muweze kuondoa tofauti zilizopo kwa kuwashirikisha wananchi ili muweze kukamilsha kipande cha barabara hii, fedha za kumalizia kipande hiki zipo”. Alisisitiza Mhagama.

Wakati huo huo, Waziri Mhagama aliuagiza Uongozi wa Wilaya ya Bagamoyo kukaa pamoja na kuandaa mfumo mzuri ambao utatumika katika kuendeshea Soko ili waweze kuanza kukusanya mapato na wananchi waweze kupata eneo la kufanya biashara pasipo na kikwazo chochote. “Ifikapo Desemba 30, 2016 soko hili liwe limekamili ili likabidhiwe kwa Halmashauri ili Januari, 2017 soko la Magomeni - Bagamoyo lianze kutumika.

Mapema: Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Hemed alisema ofisi yake itasimamia ukamilisha wa kazi hiyo na kuondoa tofauti zilizopo na kuweza kukamilisha ujenzi wa Soko ambapo kwa asilimia 98 umeshakamilika na kulikabidhi rasmi kwa wananchi pamoja na ujenzi wa kipande cha barabara kilichobakia.

-Mwisho-

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday4
mod_vvisit_counterYesterday120
mod_vvisit_counterThis week4
mod_vvisit_counterLast week825
mod_vvisit_counterThis month1889
mod_vvisit_counterLast month3455
mod_vvisit_counterAll days513524
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved