Logo
Kaya 11,000 kunufaika na Miundo Mbinu ya Kisasa Wilayani Tunduru
Monday, 20 February 2017 00:00    PDF 


Kaya 11,000 katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Songea zinatarajiwa kupata miundo mbinu ya barabara, Soko na ghala la kisasa la kuhifadhia Mpunga zitakazo wawezesha wakulima kuboresha kilimo cha Mpunga zinazojengwa kupitia program ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru, Bw. Abdallah Mussa katika ziara ya wataalamu kutoka kwenye program hiyo Februari, 2017 walipotembelea kuona utekelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu hiyo.

Bw. Mussa alisema kuwa, “program ya MIVARF, inatekeleza miradi kama hii nchi nzima na Tunduru imekuwa sehemu ya utekelezaji wa program hiyo, ambapo wakulima watanufaika na kuongeza tija katika kilimo cha zao la Mpunga uzalisha upo kwa kiwango cha juu ila changamoto kubwa ilikuwa katika usafirishaji, sehemu ya kuhifadhi mazao na soko la kuuzia bidhaa hiyo, hivyo kwa ufadhili huu wa MIVARF wakulima watanufaika sana”.

“Jumla ya Km 12 za barabara zitajengwa na mradi, ghala la kuhifadhia mpunga zaidi ya tani 1000, mashine ya kukobolea mpunga pamoja na soko vitainua uchumi wa Tunduru na kuongeza thamani ya mchele wetu kuwa wa viwango hata kuweza kuuza nchi za jirani”, alisisitiza Bw. Mussa.

Awali, wakulima walikuwa wanazalisha mazao kwa mwingi mahali pa kuhifadhia na kuuzia ilikuwa ni changamoto kubwa, hivyo Serikali kupitia Mradi wa MIVARF kwa kutuletea miundombinu hii italeta manufaa makubwa kwa wakulima, zao la mpunga litapanda bei na kuongeza thamani kwa kuzalisha mchele safi na wenye viwango,alisema Bw. Mussa.

Mratibu wa MIVARF Tunduru Bw. Method Pili amesema kati ya kata tano zitakazo nufaika na miundombinu ya masoko ni pamoja na kata ya sisi kwa sisi, Mlingoti magaribi, Nakayaya, Mtina na Namalumba  ambazo zitanufaika na miundombinu ya masoko kwani wakulima wamekuwa wakizalisha kwa kiwango kikubwa zao la mpunga lakini hawana miundombinu bora ya kutumia katika kilimo chao.

Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ni program ya miaka saba ambayo utekelezaji wake umeanza rasmi mwaka rasmi 2011. Programu hiyo inagharamiwa na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya KIlimo (IFAD), na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu. 

-Mwisho-

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday4
mod_vvisit_counterYesterday120
mod_vvisit_counterThis week4
mod_vvisit_counterLast week825
mod_vvisit_counterThis month1889
mod_vvisit_counterLast month3455
mod_vvisit_counterAll days513524
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved