Logo
Wednesday, 05 April 2017 00:00    PDF 

Waziri Mkuu akaribisha Waisraeli waje kuwekeza nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Israel waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo.

Ametoa kauli leo (Jumatano, Aprili 5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Mheshimiwa Yahel Vilan, 0fisini kwake Bungeni mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri kwa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama watalii kwa sababu kuna fursa nyingi za utalii ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na mbuga nyingi zilizosheheni wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Vilan  ameipongeza Serikali kwa utendaji wake, ambapo amesema viongozi wa makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja nchini mwaka huu kushiriki katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya Tanzania na Israel.

Amesema mbali na kushiriki katika jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo watapata fursa ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Pia Balozi Vilan amesema Serikali ya Israel itaimarisha kitendo cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.

-ends-

 

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday8
mod_vvisit_counterYesterday128
mod_vvisit_counterThis week262
mod_vvisit_counterLast week1028
mod_vvisit_counterThis month3353
mod_vvisit_counterLast month4531
mod_vvisit_counterAll days475762
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved