Logo
Kampeni ya Kitaifa ya Kuongeza uwajibikaji katika kuboresha Hali ya Lishe Nchini kuzinduliwa.
Thursday, 25 July 2013 08:22    PDF 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atazindua Kampeni ya Taifa ya kuongeza uwajibikaji katika kuboresha hali ya lishe nchini mnamo tarehe 16 Mei 2013, katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Kauli Mbiu ya Kampeni hiyo ni: Lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Taifa: Timiza wajibu wako.


Akiongea na waandishi wa habari Ikulu tarehe 9 Mei 2013, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo alieleza kuwa hali ya lishe nchini ya watoto wachanga na wadogo, wanawake walioko kwenye umri wa kuzaa na jamii kwa ujumla hairidhishi.


kwa mantiki hiyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho kikwete, ameamua kuwa mstari wa mbele katika kuongoza harakati za kuboresha hali ya lishe nchini.


Aidha, Lyimo alibainisha kuwa tatizo la utapiamlo limeendelea kuathiri jamii ya Watanzania. Hali hii imechangia kupunguza kasi ya kuelimika, kuzalisha kwa tija na hatimaye kuongezeka kwa umasikini na kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo kiuchumi na kijamii.


“Ni muhimu kujua kwamba madhara yoyote yanayoweza kutokea katika ukuaji wa kimwili kiakili kwa mtoto kutokana na udumavu, katika kipindi cha tangu mimba inapotungwa mpaka mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili yaani siku 1000 hayatarekebishwa kamwe” alisema Lyimo.


Lyimo alifafanua kuwa Takwimu za mwaka 2010 zinaonesha kuwa asilimia 42 ya watoto walio na umri chini ya miaka 5 wamedumaa; asilimia 16 wana uzito pungufu na asilimia 5 wamekonda, asilimia 59 ya watoto wenye umri kati ya miezi 6-59 wana upungufu wa damu, asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa Vitaminini A.


Aliongeza kuwa asilimia 11 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa yaani miaka 15-49 wamekonda, asilimia 41 ya wanawake wana upungufu wa damu na asilimia 58 ya wanawake wajawazito wana upungufu wa damu. Ile hali asilimia 40 ya wanawake wanaonyonyesha na asilimia 45 ya wanawake wajawazito wana upungufu wa Vitamini A.


"Ili kukabiliana na matatizo hayo na ili kutekeleza azma hii, Mhe Rais anatoa wito kwa wananchi kwa ujumla, watendaji, wanasiasa, wanaharakati, wanataaluma, viongozi wa dini, na wote kwa kushikamana koungeza uwajibikaji katika kukabiliana na tatizo la utapia mlo hapa nchini” alisisitiza Lyimo.


Lyimo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika maonesho yatakayoyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam tarehe 15 Mei, 2013 na kufikia kilele siku ya tarehe 16 Mei 2013 ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Taifa Viwanjani hapo.


Siku hiyo pia itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mikoa na Wiaya wadau wa maendeleo, taasisi zisizo za serikali, sekta binafsi na viongozi wa dini.


MWISHO.

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday105
mod_vvisit_counterYesterday117
mod_vvisit_counterThis week284
mod_vvisit_counterLast week825
mod_vvisit_counterThis month2169
mod_vvisit_counterLast month3455
mod_vvisit_counterAll days513804
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved