Logo
Tuesday, 01 August 2017 00:00    PDF 

Waziri Mkuu azuru viwanda vya Pepsi na marumaru Mbeya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha SBC Tanzania Ltd kinachotengeneza vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (marumaru) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd vya jijini Mbeya.

Amevitembelea viwanda hivyo kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa viwanda nchini, ambayo ndiyo kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano. Waziri Mkuu alivitembelea viwanda hivyo vilivyoko katika eneo la Iyunga, jijini Mbeya, jana jioni (Jumatatu, Julai 31, 2017), akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Akiwa katika kiwanda cha Pepsi, Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa kiwanda hicho kinachotarajia kuanza uzalishaji wa vinywanji baridi kwenye chupa za plastiki, ambapo amewasihi Watanzania wapende kutumia bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani.

Pia Waziri Mkuu aliishauri kampuni hiyo iendelee kupanua uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya uwekezaji. Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina wafanyakazi 190.

Nawashauri muendelee kuwekeza hapa nchini kwani mbali na utulivu wa kisiasa, pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.”

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya SBC Tanzania Ltd, Bw. Atif Dar alisema kiwanda cha Mbeya ni cha pili kwa ukubwa wa mauzo ya vinywaji baridi vinavyotengenezwa na kampuni hiyo kikitanguliwa na kile cha Dar es Salaam.

Alisema kwa sasa wanachukua soda zilizofungwa katika chupa za plastiki kutoka kwenye kiwanda chao cha Dar es Salaam, ambapo waliamua kupanua kiwanda hicho ili waanze kutengeneza soda zilizofungwa kwenye chupa za plastiki mkoani Mbeya baada ya mahitaji kuongezeka.

Bw. Dar alisema gharama za uwekezaji huo ni dola za Marekani milioni 3.5, ambapo mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi Novemba 2017 ambapo mbali na kuuza katika soko la mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pia watasafirisha katika nchi za Zambia na Malawi.

Pia Bw. Dar alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mchango wa kiwanda hicho katika uboreshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii.

Mapema asubuhi, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd na kusema kuwa mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.

Pia aliwataka Watanzania wote hususani mashirika, taasisi, asasi na mamlaka za Serikali wajenge utamaduni wa kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini ili viweze kuimarika na kusaidia kutatua tatizo la ajira.

Alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (marumaru) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, kilichoko katika eneo la Iyunga mjini Mbeya. Kiwanda hicho kinatumia malighafi za hapa nchini.

Waziri Mkuu alisema mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.

-ends-

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday46
mod_vvisit_counterYesterday124
mod_vvisit_counterThis week516
mod_vvisit_counterLast week867
mod_vvisit_counterThis month2634
mod_vvisit_counterLast month3157
mod_vvisit_counterAll days517426
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved