Logo
Friday, 28 July 2017 00:00    PDF 

Tanzania kuendeleza ushirikiano na India - Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 28, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la India, Bw. Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchi ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu na ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

“Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”

Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India watembelee maeneo ya utalii nchini ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.

Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.

-ends-

 

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday69
mod_vvisit_counterYesterday121
mod_vvisit_counterThis week69
mod_vvisit_counterLast week867
mod_vvisit_counterThis month2187
mod_vvisit_counterLast month3157
mod_vvisit_counterAll days516979
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved