Logo
MIVARF YAWEZESHA HALMASHAURI 73 KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO
Wednesday, 30 August 2017 00:00    PDF 


Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF), imefanikiwa kupunguza umasikini wa kipato na kuimarisha uhakika wa chakula katika Halmashauri 73 zinazotekeleza programu hiyo kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF wa siku mbili tarehe 29 hadi 30, Agosti, 2017  mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery alifafanua kuwa lengo la Programu hiyo ni kuongeza uzalishaji na tija kwa walengwa hasa wakulima  walioko Vijijini.

“Programu imepanga kuwajengea uwezo wazalishaji ambao huwa katika vikundi kwa kuvifiki vikundi 2,331 vyenye walengwa 81,677. Kimsingi Programu imelenga kumuwezesha mkulima aweze kufanya  kilimo cha kibiashara” alisema Assery.

Mratibu wa Programu Taifa, Walter Swai alibainisha kuwa, Programu imelenga kuwajengea uwezo walengwa kuyafikia masoko kwa uhakika ili waweze kupata sehemu ya kuuzia mazao yao na kuwasaidia kupunguza umasikini wa kipato.

“Programu imelenga kuboresha 1,000km za  barabara hadi sasa 9991.8km zimeshakamilika sawa na asilimia 92. Lakini pia kwa upande wa miundo mbinu ya masoko tunajenga maghala, hadi sasa kati ya maghala 29 yaliyo kwenye malengo, tayari tumekamilisha maghala 24 sawa na asilimia 83 ” alisistiza Swai.

Swai aliongeza kuwa Programu hiyo imepanga kukarabati maghala 6 ambapo tayari yote yamekamilika, pia tumelenga  kujenga masoko 16 ambapo hadi sasa masoko 7 yamekamilika ambayo ni asilimia 44.

MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday46
mod_vvisit_counterYesterday124
mod_vvisit_counterThis week516
mod_vvisit_counterLast week867
mod_vvisit_counterThis month2634
mod_vvisit_counterLast month3157
mod_vvisit_counterAll days517426
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved