Logo
Monday, 06 November 2017 00:00    PDF 

‘Watakaokwamisha malipo ya korosho kukiona’

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote watakaokwamisha malipo ya wakulima wa zao la korosho.

“Hatutamuacha mtu yeyote atakayesababisha wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao. Tutawakamata wote na kuwachukulia hatua stahiki.”

Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao ni lazima walipwe fedha zao kwa wakati na asitokee mtu wa kuzitamani fedha hizo. “Mkulima amelima mikorosho mwenyewe, ameokota na kukodoa mwenyewe, wao wamepewa dhamana ya kuziuza, hivyo wahakikishe wanawapelekea fedha zao na wala wasizitamani.”

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi wahakikishe mkulima hakosi sh. 3,500 katika kilo moja ya korosho atakayoiuza baada ya kukatwa michango.

Alisema bei ya juu ya korosho katika minada ya mkoa wa Lindi sh. ni 3,970 na ya chini sh. 3,800. “Vyovyote itakavyokuwa, mkulima hawezi kukosa sh. 3,500. Viongozi wa AMCOS mnisikie,” alionya.

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na kupanda kwa bei ya korosho pamoja na kupungua kwa makato ya mkulima ambapo kwa sasa hayazidi sh. 300 kwa kilo moja.

-ends-

 

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday39
mod_vvisit_counterYesterday124
mod_vvisit_counterThis week461
mod_vvisit_counterLast week825
mod_vvisit_counterThis month2346
mod_vvisit_counterLast month3455
mod_vvisit_counterAll days513981
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved