Logo
SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMA YA BUNGE MASUALA YA UKIMWI
Tuesday, 14 November 2017 12:21    PDF 

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imedhamiria kuendelea kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi ili iweze kushiriki vyema katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

Akizungumza wakati wa Semina ya siku tatu iliyoanza leo tarehe 14 Novemba, 2017 mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi inafanikiwa ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.

“Serikali imejipanga kuhakikisha swala hili linapewa kipaumbele hasa katika kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI” Alisisistiza Mhe. Mhagama

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi ni ya kila Mtanzania hivyo ni vyema wadau wote wakashirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi Mhe. Daniel Mtuka amesema  Warsha hiyo inajenga msingi kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake.

Aliongeza kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na Ukimwi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa  malengo yakuondoa janga hilo hapa nchini yanatimizwa kwa wakati muafaka.

Kwa Upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Mhe. Martha Mlata amesema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Janga la Ukimwi kwa kusimamia maadili katika Jamii hali itakayochochea kuleta mabadiliko.

Warsha hiyo ya Siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Ukimwi inafanyika mjini Dodoma ikilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.

-Mwisho-

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday45
mod_vvisit_counterYesterday124
mod_vvisit_counterThis week515
mod_vvisit_counterLast week867
mod_vvisit_counterThis month2633
mod_vvisit_counterLast month3157
mod_vvisit_counterAll days517425
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved