Logo
SERIKALI YAAZIMIA KUBORESHA MAZINGIRA YA BAISHARA NA UWEKEZAJI NCHINI
Tuesday, 30 January 2018 00:00    PDF 


Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kuweka mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na kuondoa urasimu usio wa lazima .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mashauriano baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi Prof. Faustin Kamuzora alisema leo tarehe 30 Januari, 2018 katika Ukumbi wa MIkutao wa JNICC Dar es Salaam, mkutano huu ni ushahidi kwamba Serikali na Sekta Binafsi ni wadau muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kwamba mazingira wezeshi ya biashara na kichocheo muhimu katika jitihada za Serikali kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.

“Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya BIashara na Uwekezaji (Roadmap for Improvement of Business Environment and Investment Climate in Tanzania), utekelezaji wa Mpangokazi huu utaiwezesha nchi yetu kufikia malengo yake ya kujenga uchumi wa viwanda,  ma kuongeza fursa za ajira na kuiwezesha Sekta Binafsi kuchangia katika ukuaji wa uchui na kuwa nchi ya kiapto cha kati ifikapo mwaka 2025”, Alisema Prof. Kamuzora.

Prof. Kamuzora alieleza kuwa, miongoni mwa maboresho yaliyofanyiwa kazi na Serikali ni pamoja na kuboresha mfumo wa usajili wa biashara na kampuni kwa kuanzisha mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (On-line Registration System)utakao azna kutumika hivi karibuni pamoja na kuimarisha mfumo wa usimamizi wa ardhi kwa kuanzisha mfumo unganishi wa kielektroniki wa utunzaji wa kumbukumbu  kwenye masjala ya ardhi ( Integrated Land Management Information System) na kuongeza ufanisi katika utendaji bandarini kwa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na utoaji wa huduma kwa wasafirishaji wa shehena.

Ni dhahiri kwamba dhana ya kuboresha mazingira ya biashara siyo zoezi la mara moja bali jitihada endelevu zinazohusisha ubunifu kulingana na mabadiliko kwenye ulimwengu wa kibiashara na mahitaji ya nyakati. “Napenda kutoa rai kwa waratibu wa mazingira ya biashara kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kutumia fursa ya mkutano huu kujifunza  kutoka kwa wadau wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa kuzingatia kazi na ufanisi wa biashara”, alisema Kamuzora.

Tumeunda kikosi kazi cha taifa cha uanzishwaji wa mfumo wa “Building codes” za nchi nzima ili kuweza kufanikisha mashirikiano haya baina ya sekta uuma na sekta binafsi kwa haraka na itasaidia kuleta ubunifu kulingana na mabadiliko kwenye ulimwengu wa kibiashara na mahitaji ya nyakati, alisisitiza Kamuzora.

Uchambuzi wa awali wa taarifa ya wepesi wa kufanya biashara ya mwaka 2018 umeonesha kwamba Wizara na Taasisi za Serikali zina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na mazingira rafiki na yanayotabirika ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje na kuiwezesh seta binafsi kuongeza fursa za ajira.

Mkutano huo wa siku moja umelenga kuleta mikakati bora itakayoiwezesha Tanzania kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara baina ya Sekta a Umma na Sekta Binafsi , hiini pamoja na kuboresha mazingira ya kutoa huduma kwa sekta binafsi tutakuwa tumeshiriki kikamilifu katika kulifikia azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kama inavyoelekezwa kwenye Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2017-2020/21.

Mwisho.

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday82
mod_vvisit_counterYesterday106
mod_vvisit_counterThis week291
mod_vvisit_counterLast week798
mod_vvisit_counterThis month2448
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days524633
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved