Logo
Saturday, 03 February 2018 00:00    PDF 

Majaliwa: Serikali kuimarisha masoko ya mazao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima wapate tija.

Aliyasema hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Alisema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masokoya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi. “Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija kwa mazao wanayolima.”

Alitoa mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamejipanga vema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanza na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”

Alisema kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa Stakabadhi za Mazao Ghalani kunategemea sana msaada wa Serikali. “Soko la Bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”

Bw. Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, wana imani kubwa kwamba soko hilo litatimiza malengo yake.

-ends-

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday82
mod_vvisit_counterYesterday106
mod_vvisit_counterThis week291
mod_vvisit_counterLast week798
mod_vvisit_counterThis month2448
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days524633
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved