Logo
MIVARF YACHOCHEA TANZANIA YA VIWANDA
Thursday, 22 March 2018 00:00    PDF 

Serikali kupitia Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha vijijini (MIVARF) imeweza kuinua maisha ya wananchi wa Vijijini katika Wilaya ya Meru na Mbulu Mkoani Arusha katika kuongeza thamani ya maziwa na kilimo cha vitunguu saumu.

Akizungumza na wataalamu kutoka MIVARF Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grand Demam Deo Temba alisema, tulikuwa tunasindika maziwa lita 300 kwa siku ambayo yalikuwa ni maziwa machache kulingana na uhitaji wa wananchi,  lakini sasa tunaweza kusindika maziwa 2500 kwa siku baada ya kupata uwezeshaji  kutoka MIVARF kwa kutujengea chumba cha Baridi  yaani Cold Room.

“Tangu kujengwa kwa chumba cha baridi tumeweza kuongeza bidhaa za maziwa kupitia vikundi 15 ambapo katika vikundi hivyo vina idadi ya watu 120-150 inayofikia idadi ya watu 2026 wanaoleta maziwa kiwanda”, alibainisha Temba.

Kiwanda cha The Grand Demam.co.Ltd kimeweza kuwaunganisha wafugaji  na kiwanda kwani kiwanda kinawapatia elimu ya jinsi ukamuaji wa maziwa kwa tija ili waweze kupata maziwa bora na mengi pamoja na ufugaji bora kwa kuwa na mifugo michache na kutoa maziwa mengi na kuwapa huduma za matibabu kwa mifugo yao.

Mkulima kutoka katika Wilaya ya Meru  Hilda Mroso alieleza kuwa, hapo awali alikuwa akikamua maziwa mengi lakini alipeleka lita 300 za maziwa katika Kiwanda cha The Grand Demam  kutokana na ukosefu wa mahali pa kuhifadhia, kwa sasa anauwezo wa kupeleka maziwa lita 800 kwenye Kiwanda hicho kutokana na kuongeza sehemu ya kuhifadhia maziwa hayo.

Aidha, Programu ya MIVARF pia imekiwezesha kiwanda cha Kusindika Vituguu cha Bashay Wilayani Meru kwa kuwapatia mashine ya kukaushia vitunguu ambapo hapo awali walikuwa wakikausha vitunguu kwa kutumia jua au Solar Drier iliyokuwa ikiwachukulia muda wa  wiki moja hadi sita kukausha vitunguu hivyo.

Mkulima wa zao la Vitunguu Boniface John alieleza, kabla ya uwezeshaji wa Programu ya MIVARF Kiwanda cha Kusindika Vitunguu cha Bashay  kilikuwa kinasindika kwa shida sana na kwa muda mrefu na kusindika vitunguu vichache sana.

“Upatikanaji wa Mshine hii ya kukaushia vitunguu, imekiwezesha kiwanda chetu kuboresha huduma za usindikaji kwani mashine inauwezo wa kukausha Tan moja hadi mbili za Vitunguu saumu kwa masaa nane sawa sawa na gunia 20, hivyo tunaweza kukausha kwa haraka, na imetusaidia kuongeza wateja kwani tuna kamilisha oda zetu kwa wakati haya ni maendeleo makubwa sana katika Kijiji chetu cha Bashay, alisema Mkulima huyo. ”

Kiwanda hicho kwa sasa kinauwezo wa kuuza bidhaa iliyoongezwa thamani kwa kuuza kitungu saumu kilicho sagwa yaani unga na rojo ya vitunguu saumu imewasaidia kuuza kwa urahisi na  kujiongezea kipato.

MIVARF; ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB). Lengo kuu la Mpango huu ni kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwesha kaya za vijijini kujiongeza kipato na usalama wa chakula.

MWISHO.

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday16
mod_vvisit_counterYesterday120
mod_vvisit_counterThis week496
mod_vvisit_counterLast week810
mod_vvisit_counterThis month2993
mod_vvisit_counterLast month3838
mod_vvisit_counterAll days521623
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved