Logo
WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.
Thursday, 12 April 2018 00:00    PDF 

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendela kuliombea Taifa ili kudumisha Amani na Utulivu uliopo.

Ametoa pongezi hizo hii leo alipokutana na Uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza Serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

“Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo.”Alisema Waziri Mhagama

Aliongezea kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wetu wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kufikia azma yake ya  “Tanzania ya Viwanda”.

“Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu Uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na Viongozi wote kwa ujumla wao ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo.”Alisisitiza Waziri Mhagama
Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika Huduma za kijamii hususan kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na Shule, Vyuo na Zahanati zinazohudumia Wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.

“Ni vyema sasa mkawa na mipango endelevu ya kuboresha Taasisi zenu ikiwemo Chuo cha Mount Meru na shule zenu ili kuendelea kutoa huduma za kielimu, afya ili kuwa na Watanzania wenye uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.”Alisisitiza Waziri.

Aidha kwa upande wake  Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.

“Binafsi ninaipongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa juhudi zake pamoja na uongozi wote na tunaahidi kuendelea kuwaweka mikononi mwa Mungu ili kuwa na nchi yenye Amani, Upendo, Mshikamano na Utulivu.”Alisisitiza Askofu Manase.

Mwisho.

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday81
mod_vvisit_counterYesterday106
mod_vvisit_counterThis week290
mod_vvisit_counterLast week798
mod_vvisit_counterThis month2447
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days524632
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved