Logo
WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI - IRINGA
Saturday, 14 April 2018 00:00    PDF 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Ametoa kauli hiyo Aprili 14, 2018 baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Maandalizi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Waziri amesema Kamati ya Mkoa imefanya vizuri hatua iliyomfanya kuridhishwa na maandalizi hayo.

“Nitoe pongezi kwa hatua hizi za awali mlizoanza nazo ikiwemo Kuunda kamati hii ya kuratibu shughuli zote ili kuhakikisha sherehe hizi zinafana na kuvunja rekodi.”Alisema waziri.

Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na wananchi watakaojitokeza kwa kuzingatia jiografia ya Viwanja vya Samora.

“Niwaombe mzingatie namna bora ya kuwaratibu wageni watakaohudhuria, na kuangalia namna ya kuwapanga wananchi kwa kuzingatia uwanja huu umezungukwa na wakazi wengi hivyo tunatarajia ugeni mkubwa.”Alisisitiza Waziri.

Sambamba na aliwaomba waendelee kuhabarisha umma ili Wananchi wafike kwa wingi ikiwemo Wajasiliamali wadogo ili kupata fursa ya kujitangaza na kuonesha namna mkoa unavyozalisha na kuchangia katika uchumi wa viwanda.

Aidha kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza aliahidi kusimamia vyema maandalizi na shughuli zote kwa ufanisi na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa.

“Ninaahidi kusimamia vyema yote uliyoelekeza na kutekeleza kwa ufanisi, na tunakupongeza kwa kutembelea kuangalia namna tunavyoendelea na maandalizi, nikuhakikishie tumejipanga kama Askari vitani, wakati wote tu tayari.”Alisisitiza Mhe. Masenza

Mwisho.

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday81
mod_vvisit_counterYesterday106
mod_vvisit_counterThis week290
mod_vvisit_counterLast week798
mod_vvisit_counterThis month2447
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days524632
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved